UTANGULIZI
.   .
 

UTANGULIZI
Shirika la Magereza lilianzishwa mwaka 1983 kwa Sheria ya Bunge namba 23 ya mwaka 1974 (the Corporation Sole Act No. 23/1974) chini ya kifungu cha 3(1) na kanuni zake za mwaka 1983.

DIRA
Shirika linajizatiti kuendesha shughuli zake kibiashara kuzalisha mali kwa ubora katika mzingira ya ushindani ili kupata faida.

MWELEKEO
Bado tunalo lengo la kuboresha zaidi miradi ya Shirika ili iwe na uwezo kiuzalishaji na kuimarisha manejimenti ya miradi katika mwelekeo wa kuwa na miradi yenye tija na ufanisi.

MALENGO
(i) Chombo cha urekebishaji wafungwa kuwafundisha stadi za kazi na kuwaongezea ujuzi kwa wale ambao tayari wana ujuzi.

(ii) Kuendesha shughuli zake kiuchumi na kibiashara kwa kujitegemea (Revolving fund).

(iii) Kuipunguzia Serikali mzigo wa gharama za uendeshaji wa Magereza.