Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango(wa tatu toka kulia) akipokea mfano wa hundi ya Tsh. 130,000,000 ikiwa ni gawio la Shirika la Magereza (SHIMA) toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Magereza, Meja Jenerali Mstaafu, Raphael M. Muhuga (kulia) Desemba 12, 2019 jijini Dodoma. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo DCP. Afwilile M. Mwakijungu.