TANGAZO LA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA KAMPUNI YA ULINZI YA SHIMA

 (SHIMA GUARD Co Ltd) TAREHE 28/05/2021

SHIMA GUARD – Ni Kampuni tanzu ya Shirika la Magereza linalotarajia kutoa nafasi za Ajira Ya Ulinzi hivi karibuni, ili uweze kuajiriwa na kampuni tajwa ni lazima uwe umepitia mafunzo yanayoendeshwa na kampuni hiyo bila malipo.  Aidha, kampuni inatangaza nafasi za mafunzo hayo kwa wenye sifa zifuatazo:-

  View pdf file here      

 • Awe raia wa Tanzania
 • Awe na umri wa miaka 20 - 40
 • Awe hajawahi  kuhukumiwa au kuwa na rekodi ya makosa ya jinai
 • Awe na elimu ya kuanzia darasa la saba hadi kidato cha sita
 • Awe na tabia njema
 • Awe anajua kusoma  na kuandika Kiswahili au Kingereza kwa ufasaha
 • Awe tayari kufanya kazi  mahali popote atakapopangiwa mara baada  ya  kumaliza mafunzo
 • Awe hana rekodi ya matumizi ya dawa za kulevya
 • Awe na akili timamu
 • Asiwe na ulemavu wa aina yoyote

 

JINSI YA KUTUMA MAOMBI

Kwa Mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani, barua za maombi ya kujiunga na mafunzo zikiwa na namba ya simu ya muombaji ziwasilishwe/zipelekwe ofisi za Kikosi Maalum cha Magereza (KMKGM) zilizopo Ukonga Magereza, Wilaya ya Ilala Dsm.

Au kwa barua pepe ifuatayo:- This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. 

 Kwa Mkoa wa Mwanza na mikoa ya jirani, barua za maombi ya kujiunga na mafunzo zikiwa na namba ya simu ya muombaji ziwasilishwe/zipelekwe ofisi za Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mwanza zilizopo Butimba, Mwanza.

Au kwa barua pepe ifuatayo:- This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.   

Kwa Mkoa wa Dodoma na mikoa ya jirani, barua za maombi ya kujiunga na mafunzo zikiwa na namba ya simu ya muombaji ziwasilishwe/zipelekwe ofisi za Kampuni ya Ulinzi ya SHIMA (SHIMA Guard Co.Ltd) zilizopo eneo la Nzunguni viwanja vya nae nane.

Au kwa barua pepe ifuatayo:- This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.  

Barua za maombi zitumwe zikiwa na viambatanisho vifuatavyo:-

 • Picha za Passport size mbili zilizopigwa hivi karibuni
 • Nakala ya cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria /Hakimu au kiapo (Affidavit original)
 • Nakala ya vyeti vya kuhitimu Elimu ya Msingi au Sekondari
 • Barua ya utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa/Kijiji sehemu anakoishi
 • Nakala ya kitambulisho chaTaifa (NIDA) au cha mpiga kura
 • Form ya uthibitisho wa afya yake kutoka Hospitali ya Serikali
 • Barua ya wadhamini wawili (02) wenye utambulisho kutoka Serikali  ya Mtaa /Kijiji zikiwa na picha mbili za wadhamini  na namba zao za simu

N.B:      Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 01/06/2021 na watakaokuwa na sifa watajulishwa.

Imetolewa na,

Mkurugenzi Mtendaji,

Kampuni ya ulinzi ya SHIMA (SHIMA GUARD Co Ltd).

S.L.P 1725,

DODOMA.