Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi ( wakwanza kushoto) akizindua rasmi Kiwanda cha Maziwa cha Magereza (Kingolwira Milk Products Industry).Kiwanda cha Maziwa cha Magereza (Kingolwira Milk Products Industry), che uwezo wa kuchakata Maziwa Lita elfu moja kwa siku kimezinduliwa rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi ( Mwenye Barakoa nyeusi) akiwasili Kiwanda Cha Maziwa cha Magereza ( Kingolwira Milk Products Industry) kwaajili ya kukizindua rasmi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akikata utepe wakati akizindua Jengo la huduma za Mama na mtoto katika kituo cha Afya cha Gereza Mtego wa Simba mkoani Morogoro.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Meja Jenerali Suleiman Mzee (kushoto) akizungumza Jambo na viongozi mbalimbali muda mfupi baada ya shughuli ya uzinduzi wa miradi ya Magereza kukamilika Mkoani Morogoro.